Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam imekubali ombi la klabu ya Yanga ya kusogezwa mbele kwa muda wa kusikilizwa kesi iliyofunguliwa na wanachama wa klabu hiyo kuhusu uhalali wa Baraza la wadhamini wa klabu hiyo.
Kufuatia hatua hiyo Mahakama hiyo itaisikiliza upya kesi hiyo na baadae maamuzi yatatolewa kuhusu kesi hiyo. Yanga itawakilishwa na jopo la mawakili wakiongozwa na wakili Simon Patric (pichana)
Awali Mahakama hiyo iliamuru Uongozi wa klabu ya Yanga ukiongozwa na Rais wa Yanga Injinia Hersi Saidi na wenzake, kuachia ngazi na kuondoka kwenye klabu hiyo kwa kile kilichodaiwa kuwa Katiba ya Yanga haitambui uwepo wao.
