Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania, Ibrahim Class, leo Aprili 15, 2026, ametembelea Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) ikiwa ni sehemu ya kupokea neno la baraka kuelekea pambano lake la marudiano la kuwania mikanda miwili ya WBC International Silver na WBC International Gold.
Pambano hilo la marudiano linatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa World Siam Stadium, jijini Bangkok, Thailand, tarehe 25 Aprili 2026.
Akizungumza na wanahabari, Kaimu Mwenyekiti wa TPBRC, Patrick Nyembera, amemtakia kila la kheri bondia huyo kuelekea pambano hilo, huku akisisitiza kuwa Watanzania wote wako nyuma yake na kumuomba arejee na mikanda yote miwili.
