WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amewasili mkoani Kigoma hii leo, Alhamisi Aprili 16, 2026, ambako anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji la Ziwa Tanganyika (Lake Tanganyika Business and Investment Forum).
Kongamano hilo linawakutanisha viongozi wa Serikali, wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchi zinazozunguka ziwa Tanganyika, zikiwemo Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Tanzania ambayo ni mwenyeji wa kongamano hilo lililoanza jana Jumatano, Aprili 15 ambapo litatamatika Jumamosi, Aprili 18, 2026.
Akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kigoma, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu amepokelewa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Simon Sirro. (Picha na OWM)


