Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, amemteua tena makamu wake wa zamani, James Wani Igga, kushika wadhifa huohuo. Shirika la utangazaji la linalomilikiwa na serikali ya nchi hiyo limetangaza hayo.
Hatua hiyo imejiri baada ya Kiir kumfuta kazi mshirika wake mwenye ushawishi mkubwa ambaye alikuwa akionekana kama ambaye angekuwa mrithi wake wa baadaye.
Hofu ya kurejea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe inaongezeka katika taifa hilo changa zaidi duniani, huku kukiwa na hali ya sintofahamu kuhusu nani atakuwa mrithi wa Salva Kiir mwenye umri wa miaka 74, ambaye mara kwa mara amekuwa akiwafuta kazi, kuwarejesha, na wakati mwingine tena kuwatimua maafisa waandamizi.
Wachambuzi wanaona hatua hizo kama juhudi za kutuliza makundi mbalimbali ya kisiasa na kupita katika nyakati za kisiasa zenye misukosuko
