Russian President Vladimir Putin gives a speech at a meeting of advisory council of the Russian parliament in Saint Petersburg on April 27, 2022. (Photo by Alexey DANICHEV / SPUTNIK / AFP)

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov amekanusha uvumi kuwa rais Vladimir Putin ni mgonjwa.
Katika mahojiano na TV ya Ufaransa, Lavrov amesema kiongozi huyo wa Urusi anaonekana hadharani kila siku, na hakuna mtu mwenye akili timamu angeona dalili zozote za ugonjwa.
Kumekuwa na uvumi unaoongezeka wa vyombo vya habari ambao haujathibitishwa kwamba Putin, ambaye anatimiza miaka 70 mwaka huu, anaweza kuwa na afya mbaya, labda anaugua saratani.
Mahojiano hayo yanajiri huku Urusi ikiendelea na kasi yake ya mashambulizi katika eneo la Donbas nchini Ukraine.
Lavrov alisema “ukombozi” wa eneo la mashariki ni “kipaumbele kisicho na masharti” kwa Urusi.
Alirudia madai ya Kremlin kwamba Urusi inapigana na “utawala wa Nazi-mamboleo”.
