
Mamlaka ya udhibiti ya magonjwa nchini Nigeria (CDC), imetangaza uwapo wa visa vipya 6 vya ugonjwa wa Monkeypox.
Wagonjwa wapya waliothibitshwa mwezi huu wa Mei, 2022, ni kutoka majimbo manne ya Bayelsa (2), Adamawa (2), Lagos (1) na Rivers (1).
Kwa ujumla nchi hiyo imethibitisha visa 21 tangu kuuka kwa ugonjwa huo umwaka huu, na kifo kimoja cha mgonjwa aliyekuwa na umri wa miaka 40.
Visa vyote 21 vimeripotiwa katika majimbo tisa na mji mkuu wa Abuja.
Kabla ya kuingia Afrika, janga la Virusi hivyo lilianza kubainika barani Ulaya, Australia na Marekani.
