Moto mkubwa uliozuka saa 8 usiku wa kuamkia leo Mei 30, 2022, umeteketeza soko la Vetenari lililopo eneo la Tazara, jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa zimamoto na uokoaji, mkoa wa Temeke, Michael Bachubira, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Licha ya kuwa hadi sasa chanzo cha moto huo hakijafahamika, lakini jitihada za kuuzima zilifanikiwa.
Kumekuwa na muendelezo wa matukio ya masoko kuungu moto jijini Dar es Salaam ambapo kwa mwaka huu pekee masoko ya Mbagala na Karume nayo yameungua.
