
Wanawake na mabinti 16 wa mtandao unaojihusisha na vitendo vya ngono kwa kutumia vifaa hatarishi kama chupa za soda na bia, mahindi ya kuchoma, ndizi na matango wamenaswa na kutiwa mbaroni.
Watu hao wamekamatwa mwishoni mwa wiki maeneo ya Mwananyamala, Kinondoni Mkwajuni, Tandale, Sinza, Buza na Magomeni jijini Dar es Salaam.
Vyombo vya dola na mamlaka husika vinaendelea kukamilisha taratibu za kisheria ili wafikishwe mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.
Kukamatwa kwa watu hao kumekuja baada ya uchunguzi uliofanywa na vyombo vya dola ambao ulibaini kuibuka kwa baadhi ya wanawake wanaofundishana kufanya vitendo vya ngono kwa kutumia vifaa hivyo.
Baadhi wameunda makundi ya WhatsApp ili kuweka picha zao za utupu na wengine huziweka katika mitandao tofauti ya kijamii.
Uchunguzi zaidi umebaini kuwa wanawake na mabinti wanaoonekana kukubuhu kufanya vitendo hivyo husafirishwa kwenda ughaibuni na kutumikishwa katika biashara ya ukahaba, jambo ambalo ni kinyume cha sheria za Tanzania.
Rais Samia Suluhu Hassan, katika hotuba yake ya Mei 3, 2022, alipokuwa akifungua Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, yaliyofanyika kwa Bara la Afrika jijini Arusha, aligusia kuporomoka kwa maadili hapa nchini.
Alitumia jukwaa hilo kuelekeza viongozi kusimamia suala la maadili nchini. Baada ya agizo hilo la Rais, Waziri Mku, Kassim Majaliwa alizielekeza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wanawake Wazee, na Makundi Maalum, kushirikiana kukabiliana na uovu huo na hivyo zimefanikiwa kuwanasa washukiwa hao.
