
Mazishi ya mtoto Zaurati Shaban mwenye umri wa miaka 2.8, aliyeuawa na tembo katika kijiji na kata ya Ntuntu, wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, yamenyika mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Jerry Muro aliongoza waombolezaji katika mazishi hayo.
Mtoto huyo alifariki dunia Mei 27, 2022, saa mbili asubuhi, kitongoji cha Wangama alipokwenda kuteka maji kisimani pamoja na mama yake.
DC Muro baada ya kufikia msibani alitoa pole kwa wazazi wa marehemu na wananchi wa kata ya Ntuntu na kuwahakikishia kuwa wataalam wa idara ya wanyamapori wataweka kambi eneo hilo hadi hatma ya tembo huyo itakapojulikana.
