- Spika Tulia amfagilia Rais Samia

Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma.
Dk. Tulia amesema jambo hilo siyo dogo kwa ustawi wa nchi hasa ukizingatia changamoto wanazozipitia wafanyakazi.
Kwa upande mwingine Dk. Tulia amempongeza Rais Samia kwa kitendo chake cha kuitangaza nchi kupitia filamu ya The Royal Tour kwani kwa kufanya hivyo amesaidia kutangaza utalii na ni jambo ambalo amelifanya kwa vitendo.
Spika Dk. Tulia amegusia pia ziara ya Rais Samia mkoani Tabora ambako alifanikiwa kuzindua barabara yenye urefu wa kilomita 342.9 inayotoka Tabora hadi Mpanda pamoja na barabara nyingine iliyopo ndani ya mkoa wa Tabora, akibainisha kuwa hatua hiyo ni muhimu sana kwa maendeleo ya mkoa lakini kwa ukuaji na ustawi wa uchumi wa nchi nzima.
Dk. Tulia ameyasema hayo wakati alipopewa nafasi ya kuzungumza wakati wa hafla ya uapisho wa wateule mbalimbali katika nafasi za Wenyeviti wa Bodi na Watendaji wa Taasisi mbalimbali, iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma.
