
Gari aina ya Toyota Pickup lenye namba za usajili T 840 DQF limegonga behewa la Treni mkoani Morogoro.
Gari hilo lililokuwa likitokea maeneo ya Tumbaku kuelekea Msamvu liligonga treni hiyo iliyokuwa ikitokea Kilosa kuelekea Stesheni ya Morogoro.
Ajali hiyo iliyotokea juzi Mei 23, 2022, tayari askari wa Usalama Barabarani walishafika eneo la tukio kushughulikia uokoaji na kubaini chanzo chake.
