Basi la Kampuni Super Feo linalofanya safari zake kati ya Songea na Dar es Salaam, kupitia njia ya Lindi, limepata ajali iliyosababisha majeruhi.
Ajali hiyo ilitokea Jumapili asubuhi ya Mei 22, 2022 wakati basi hilo likipita katika kijiji cha Hulia, wilaya ya Tunduru.
Abiria kadhaa wamejeruhiwa pamoja na dereva Halima Mbwana ambaye anadaiwa kukatika mkono.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma, Joseph Konyo alithibitisha kutokea ajali hiyo.
Konyo alisema Halima mama wa watoto watatu, aliyejipatia umaarufu siku za hivi karibuni kwa kuwa dereva mwanamke anayeendesha mabasi ya abiria aliyeanzia kuwa kondakta kabla ya kwenda kusomea udereva, amekimbizwa hospitalini kwa matibabu zaidi.
