Wafuasi wa ulamaa wa kidini wa madhehebu ya shia, Muqtada al Sadr wamefyatua maguruneti kwa kutumia roketi kwenye eneo la ulinzi mkali katika mji mkuu Baghadad wakati milio ya risasi ikisikika katika eneo hilo leo Jumanne.
Wafuasi wa al Sadr wamefyatuliana risasi na vikosi vya usalama vya Iraq katika eneo hilo na televisheni imeonesha moja kwa moja makabiliano hayo, ikielezwa kwamba hadiĀ sasa Wairaq 22 wameshauawa.
Machafuko yameanza tangu jana baada ya Muqtada al Sadr kutangaza kujiuzulu siasa.
Kwa miezi sasa mamilioni ya wafuasi wa kiongozi huyo wamekuwa wakitaka bunge livunjwe na uchaguzi mpya uitishwe.
Nchi jirani ya Iran imefunga mipaka yake na Iraq na miji kadhaa ya Iraq iko chini ya amri ya kuwazuia watu kutembea.
