
Watalii wanne wa Ujerumani na rubani wa Afrika Kusini wamefariki baada ya ajali ya ndege nchini Namibia.
Ndege hiyo ilianguka jana Jumanne dakika chache baada ya kuanza safari katika uwanja mdogo wa ndege wa kisiwa cha Impalila kilicho kando ya Mto Zambezi.
Ripoti ya polisi inasema walikuwa wakisafiri kwa ndege ya kukodi aina ya Cessna 210 yenye namba ya usajili V5-LMK.
