
Mtaalam wa virutubisho tiba, Abdallah Mandai amewataka wenye maradhi ya kisukari kutumia juisi ya barungi kwa kuwa ina uwezo mkubwa wa kurekebisha kiwango cha sukari kwenye mwili wa mwathiriwa na kubaki katika hali ya kawaida.
“Tengeneza juisi kwa barungi tatu, kunywa asubuhi, mchana na jioni,” amesema mtaalam Mandai leo Jumanne Agosti 30, 2022, jijini Dar es Salaam.
“Pamoja na kutumia tiba, mazoezi ya viungo kama kutembea mwendo mrefu, kukimbia, kuogelea na ‘push up’ ni muhimu kwa mwathiriwa wa kisukari.
“Mgonjwa wa kisukari pia apendelee kula mboga za majani vikiwamo vitunguu swaumu, vitunguu maji, matango na maharagwe yasiyokomaa yanayoliwa pamoja na maganda yake,” amesema Mandai.
Mtaalam Mandai amewataka wanaosumbuka kwa magonjwa mbalimbali kwenda katika kituo chake cha kutolea huduma za afya kilichoko Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wawasiliane naye kwa simu namba 0745900600.
