*Nyaisonga atoa neno

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Mbeya, Mhashamu Gervas Nyaisonga, amewataka waamini wa kanisa hilo Tanzania, Malawi na Zambia kutoa ushirikiano kwa mamlaka ili kubaini wauaji wa mapadri wa Shirika la Wamisionari wa Afrika.
Askofu Mkuu Nyaisonga ametoa kauli hiyo leo Juni 16, 2022, jijini Mbeya wakati wa ibada ya kumwombea Padri Michael kabla ya mazishi yake kwenye makaburi ya Mwanjelwa jijini humo.
Mwili wa Padri Michael Samson wa Shirika la Wamisionari wa Afrika, ulikutwa mto Meta, eneo la Sabasaba, Juni 12, mwaka huu, baada ya kutoweka jioni ya Juni 11 alipoaga anakwenda mazoezini.
Kauli ya Nyaisonga inakuja baada ya Padri Michael raia kutoka nchi jirani ya Malawi kuuawa katika mazingira ya utata kama ilivyotokea kwa Aprili 12, 2022, Padri Francis Kangwa wa Shirika hilo, raia wa Zambia naye alikutwa amefariki dunia na mwili wake kukutwa ndani ya tenki kubwa la maji lililopo nyuma ya nyumba ya makazi yao.
Amewataka waamini wa kanisa hilo kupokea msiba huo kwa imani huku wakimwombea pumziko lenye heri Mbinguni, Padri Michael.
