
Watu watatu wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa katika ajali ya basi la Zubery iliyotokea jana Juni 15, 2022, saa 8 mchana katika barabara ya Mwanza – Shinyanga eneo la Mwigumbi.
Taarifa zinasema Basi hilo liligonga ukingo wa daraja na kutumbukia bondeni na hivyo kusababisha vifo hivyo, huku mmoja wa waliofariki Hamza Katima akiwa ni dereva wa basi hilo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, George Kyando amesema taarifa za awali zinaonesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi hilo kupata tatizo la kiafya akiwa safarini.
Hivyo, ametoa mwito kwa madereva kuangalia afya zao mara kwa mara kabla ya kuanza safari ili kuepusha matukio kama hayo.
