
Michael Malanyingi
Watanzania wametakiwa kutoyumbishwa na dhana potofu kuwa chanjo ya Uviko 19 ina madhara badala yake wachukue uamuzi sahihi wa kuitumia.
Askofu Sebard Lipala wa makanisa ya Betheli Gospel Revival Church ametoa rai hiyo hivi karibuni alipokuwa akihubiri kwenye ibada ya maombi maalumu ya kuliombea Taifa liondokane na janga la korona.
“Ingawa chanjo hii imekuja kwa hiari, nikiwa kama kiongozi wa dini ninawahamashisha Watanzania tuchanje kwa faida ya Taifa letu na Dunia nzima.
“Niwatake Watanzania wasitishiwe na baadhi ya maneno yanayoogopesha na kukatisha tamaa kuwa chanjo hii siyo sahihi, huo ni upotoshaji tuendelee kujitokeza kupata chanjo,” amesema.
Askofu Lipala amesema Watanzania hawanabudi kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuwaletea chanjo ya corona hapa nchini kwani kupitia chanjo hiyo kuna uwezekano mkubwa wa kupunguza maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo nchini.
