Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Sylvester Mwakitalu, amethibitisha kuachiwa huru kwa viongozi wawili wa Jumuia za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI).

Viongozi hao walikuwa mahabusu tangu mwaka 2014 pamoja na wenzao 34 kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya ugaidi ambayo hayana dhamana.
Mwakitalu amesema amewafutia mashtaka viongozi wote wa jumuia hiyo na kilichobaki sasa ni taratibu za kutoka gerezani.
Walioachiwa huru jana Jumanne Juni 15, 2021 ni Sheikh Farid Hadi Ahmed na Mselem Ali Mselem ambao walikuwa wanakabiliwa na kesi ya ugaidi.
