Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa polisi wa jimbo la Guetang nchini humo, Mavela Masondo, imesema miili ya wanandoa hao iligunduliwa bafuni kwao Jumapili Juni 13, mwaka huu.
Ilibainika kuwa wakiwa bafuni mke alishika soketi ya umeme akapigwa shoti ambapo mume alipojitosa kumuokoa wote wakafariki dunia.
Aidha, taarifa za awali zinasema katika eneo hilo watu hupenda kujiunganishia umeme kiholela kinyume na sheria na hivyo kusababisha majanga kama hayo.
Hata hivyo, polisi wamesema bado wanaendelea kuchunguza zaidi tukio hilo kwa kushirikiana na mamlaka inayohusika kusambaza umeme katika jimbo la Guetang.
