
Mtaalam wa tiba asili na virutubisho tiba, Abdallah Mandai amefichua nguvu ya kitiba iliyomo katika majani ya ulezi, zao linalostawishwa katika mikoa mingi nchini.
Amesema majani hayo ni tiba nzuri kwa vipele vinavyofanana na malengelenge ambavyo hujulikana kama eczema.
“Pondaponda majani ya ulezi, baada ya kulainika kamua maji yake kupata juisi ya kutosha kupaka sehemu zote zilizoathirika.
“Rudia kufanya hivyo kutwa mara tatu mfululizo katika kipindi cha siku 21 utaondokana na tatizo hilo,” amesema Mtaalam huyo leo Jumatano, Septemba 14, 2022, jijini Dar es Salaam.

Aidha, ametoa mwito kwa jamii inayoteseka kwa maradhi mbalimbali, kwenda katika kituo chake cha kutolea huduma za afya, Ukonga Mongo la Ndege, jijini Dar es Salaam, au wampigie simu namba 0745900600.
