
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ametoa mwito wa kuwapo mshikamano na ushirikiano kuunusuru “ulimwengungu ulio hatarini” kutokana na mizozo, umasikini, mfumo wa kifedha ulioparaganyika na athari za mabadiliko ya Tabianchi.
Kupitia hotuba yake ya kufungua mkutano wa 77 wa hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa, Guterres amesema changamoto hizo zinazoukabili ulimwengu ni kitisho kwa juhudi za kufikiwa amani ya kudumu, haki za binadamu na maendeleo endelevu.
Mwanadiploamisa huyo mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka kuwapo hatua za pamoja na mshikamano miongoni mwa mataifa duniani kwenye kuzitafutia majibu changamoto hizo.
Hotuba hiyo ya Guterres ndiyo imefungua rasmi mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa wa kila mwaka ambao uwaleta pamoja viongozi wa nchi, serikali na wanadiplomasia mjini New York kuzungumza mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
