
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Meja Generali John Mkunda kuwa mkuu mpya wa majeshi ya ulinzi nchini, akichukua nafasi ya Jenerali Venancy Mabeyo anayestaafu hii leo.
Kabla ya uteuzi huo alikuwa mkuu wa tawi la oparesheni mafunzo makao makuu ya Jeshi hilo nchini.

