
Mtaalam wa virutubisho tiba, Abdallah Mandai amesema majani na mizizi ya mahindi ni tiba maridhawa ya maradhi ya figo na kibofu cha mkojo.
Amesema ndevu za mahindi ni dawa ya maumivu wakati wa kukojoa, zinasaidia pia kuondoa uvimbe kwenye miguu.
Mandai ameyasema hayo leo Juni 29, 2022, jijini Dar es Salaam, wakati akizungumzia mimea mbalimbali inayostawishwa na jamii kwa ajili ya chakula pia ni tiba ya magonjwa mbalimbali.
“Kwa waanaopata shida wakati wa kukojoa hususan wazee, na watoto wanaokojoa kitandani ndevu za mahindi pia ni tiba nzuri kwao.
“Chukua mizizi na majani ya mahindi vichemshe muda wa dakika 15, chuja na kunywa maji hayo.
“Chukua ndevu za mahindi za kutosha, chemsha na lita mbili za maji muda wa dakika 15, chuja kunywa glasi mbili kwa siku, muda wa siku tano.
“Unaweza pia kutumia kijiko kimoja cha mezani cha kitunguu maji kilichosagwa kuwa kama ujiuji, changanya na asali kijiko kimoja cha chai, lamba mara tatu kwa siku muda wa mwezi mmoja na nusu (majuma sita) ni dawa nyingine nzuri ya kutokojoa kitandani,” amesema Mtaalam huyo.
Aidha, Mandai ametoa mwito kwa mwenye tatizo lolote la kiafya, aende katika kituo chake cha kutolea huduma za afya, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au ampigie simu kwa namba namba 0745900600 iwapo anataka ufafanuzi wa jambo.
