Berlin, Germany - November 04: Antonio Guterres, High Commissioner for Refugees of UNHCR, attends a press conference in german foreign office on November 04, 2015 in Berlin, Germany. (Photo by Michael Gottschalk/Photothek via Getty Images)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres atakutana na viongozi wa Ukraine na Uturuki kesho Alhamis kutahmini utekelezaji wa mkataba ulioruhusu kuanza kusafirishwa tena nafaka za Ukraine na njia za kidiplomasia za kukomesha vita nchini humo.
Guterres atafanya mazungumzo katika mji wa magharibi mwa Ukraine wa Lviv na Rais Volodymyr Zelensky na mwenzake wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema watajadili kuhusu suluhisho la kisiasa kwa mzozo unaoendelea.
Guterres kisha atazuru mji wa bandari wa Odessa nchini Ukraine siku ya Ijumaa – ambayo ni mojawapo ya bandari tatu zinazotumika kusafirisha nafaka, kabla ya kuelekea Uturuki.
