
Kiongozi wa upinzani wa Urusi Alexei Navalny ametoa mwito kwa nchi za Magharibi kuwawekea vikwazo vikali mabwenyenye wa Urusi, wakati vita vya Moscow dhidi ya Ukraine vikiendelea bila kukomeshwa.
Navalny ameandika kutoka gerezani anakozuiliwa kuwa vikwazo vinahitajika ili kumlazimisha mvamizi kusitisha vita. Vinatumika kumuwekea mbinyo.
Amesema mbali na vikwazo vikali vya mafuta na gesi, ni muhimu pia kuwalenga watu binafsi.
