
Mtaalam wa tiba asili na virutubisho tiba, Abdallah Mandai amesema mimizizi ya bamia ni tiba anuwai ya tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
“Chukua gramu 10 za unga wa mizizi ya bamia, changanya na gramu 15 za unga wa mizizi ya asparagasi weka katika chombo cha kuchemshia, tia glasi moja ya maziwa kisha chemsha ndani ya dakika tano.
“Kunywa asubuhi na jioni saa moja kabla ya muda wako wa kwenda kulala. Zingatia tiba hii ni nzuri hata kwa wale ambao ni hanithi na wanaofikia kilele kwa muda mfupi.
“Tumia tiba hii katika kipindi cha mwezi mmoja mfulizo,” mtaalam Mandai ametanabahisha hilo leo Jumatatu Septemba 12, 2022, jijini Dar es Salaam.

Aidha, ametoa mwito kwa yeyote anayesumbuliwa na tatizo la aina yoyote la kiafya amwone katika kituo chake cha kutolea huduma za afya Ukonga, Mongo la Ndege, jijini Dar es Salaam, au ampigie simu namba 0745900600 iwapo anataka ufafanuzi wa jambo au namna ya kufika katika kituo hicho.
