Rais Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wageni mbalimbali pamoja na Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA), mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, jana Septemba 11, 2022 kwa ajili ya Sherehe za Miaka 50 ya WAWATA.Rais Samia Suluhu Hassan akiangalia bidhaa mbalimbali kwenye mabanda ya Maonesho ya Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA), kutoka majimbo mbalimbali nchini mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jana Septemba 11, 2022 kwa ajili ya kushiriki Jubilee ya miaka 50 ya WAWATA tangu kuanzishwa kwake.Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na maaskofu Katoliki wa majimbo mbalimbali nchini wakati wa Jubilee ya miaka 50 ya Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA), iliyofanyika jana Septemba 11, 2022 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA), wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, jana Septemba 11, 2022 katika maadhimisho ya miaka 50 ya WAWATA. Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Jubilee ya miaka 50 tangu kuasisiwa WAWATA katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, jana Septemba 11, 2022, jijini Dar es Salaam (PICHA NA MZALENDO BLOG & ONLINE TV).