
Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin, ametangaza kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona.
Hata hivyo, amesema ana dalili za kawaida na ataendelea na majukumu yake akiwa karantini nyumbani kwake muda wa siku tano zijazo.
Austin ambaye amepata dozi kamili ya chanjo na ya ziada amesema kwenye taarifa yake kwamba mara ya mwisho Desemba 21 alikutana na rais Joe Biden, ikiwa ni zaidi ya wiki moja kabla ya kuanza kuhisi dalili za maambukizi.
Taarifa hiyo inatolewa wakati Pentagon wiki iliyopita ikiimarisha vizuizi vya kudhibiti maambukizi ya COVID- 19 kwenye makao makuu yake kufuatia wasiwasi wa kusambaa kwa kasi kwa aina ya kirusi cha corona, Omicron.
Anakuwa miongoni mwa maofisa wa ngazi za juu wa Serikali ya Biden kukutwa na maambikizi ya COVID-19
