
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) pamoja na ofisi ya Umoja wa mataifa ya haki za binadamu wamesema wanawake wapatao 131 wasichana walibakwa.
Ripoti hiyo inaongeza kuwa karibu raia 200 wameuawa kwenye jimbo lililotatizika la Unity, katika muda wa miezi mitatu.
Mashirika hayo mawili yameorodhesha ukiukwaji wa haki za kimataifa za binadamu pamoja na sheria za kimataifa za haki za binadamu kwenye jimbo la Unity nchini humo.
Ukatili huo unasemekana kutokea wakati wa mapigano kati ya vikosi vya serikali vikishirikiana na makundi rafiki yenye silaha, dhidi ya vile vya SPLM/IO ambavyo ni vitiifu kwa makamu wa rais Riek Machar.
UNMISS imesema ripoti hiyo inaangazia kati ya Februari 11 na Mei 31 mwaka huu kwenye kaunti 3 za jimbo la Unity za Koch, Leer na Mayendit.
Aprili UNMISS ilisema watu wapatao 72 waliuawa Sudan Kusini, huku wasichana 64 pamoja na wanawake wakibakwa kati ya Februari na Aprili kwenye kaunti ya Leer jimbo la Unity.
