Wanandoa Paskari Ernest (46), na mkewe Jeska Bartazal (39), wakazi wa Sengerema, mkoani Mwanza, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoa huo kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wao Aneth John(8), mwanafunzi wa darasa la awali, shule ya Msingi Nyancheche.
Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Hamis Mwampelwa amedai mtoto huyo amepoteza maisha Machi 29, 2022, saa 11 jioni baada ya kupigwa na mama yake huyo mzazi.
Kamanda Mwampelwa amedai mama huyu alikuwa na desturi ya kumpiga mtoto huyo hadi kukimbia nyumba na kuhamia kwa majirani.
Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Nyancheche, Josephati Maumba, amethibitisha kuwa mtoto huyo alikuwa mwanafunzi wa darasa la awali katika shule hiyo.
