
Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa katika kikao chake kilichofanyika jana Machi 30,2022, katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete (Convention), jijini Dodoma imefanya uteuzi wa makatibu wa UVCCM wilaya na kufanya mabadiliko ya vituo vya kazi kwa baadhi ya makatibu hao wa UVCCM.
Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Kenani Kihongosi.
“Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi inapenda kuwajulisha wanachama wote wa Chama chetu na wanachama wa UVCCM kwamba, Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa katika kikao chake kilichofanyika Machi 30/2022, Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, kimefanya uteuzi wa makatibu wa UVCCM wilaya kama ifuatavyo;




