
Benki ya Dunia (WB), imepunguza kiwango chake cha makadirio ya ukuaji wa uchumi, ikitahadharisha kuwa baadhi ya nchi zinakabiliwa na mporomoko wa uchumi kwasababu ya vita ya Urusi nchini Ukraine na virusi vya corona.
Benki hiyo inasema Afrika Mashariki na baadhi ya maeneo ya Ulaya yameathiriwa zaidi.
Imesema kuna hatari kubwa kudolola kwa ukuaji wa uchumi, na ukosefu wa ajira huku mfumuko wa bei ukiongezeka – na hali hii inaweza kurejea kwa mara ya kwanza tangu miaka ya 1970, iliyosababisha kupanda kwa bei za vyakula na mafuta.
Akizungumza na BBC, Mkuu wa Benki hiyo, David Malpass, amesema ni vigumu kutazama upande mwingine wa mzozo.
Amesema baadhi ya nchi zinazoendelea zinakabiliwa na deni kubwa, huku serikali zikishindwa kununua bidhaa.
Kiwango cha makadirio ya ukuaji mpya wa uchumi wa dunia cha benki hiyo kwa sasa ni cha asilimia -2.9. Kiwango hicho kikionesha kuporomoka kwa uchumi wa dunia ambako hakujawahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 80.
