
Kansela wa Ujerumani anayemaliza muda wake, Angela Merkel, amesema suala la usalama wa Israel litaendelea kupewa kipaumbele na kila serikali ya Ujerumani.
Kansela Merkel ametoa matamshi hayo nchini Israel kwenye ziara yake ya kuagana na viongozi anapokaribia kumaliza muda wake wa uongozi wa miaka 16 madarakani.
Amesema ni hatua ya matumaini kuona Israel hatimaye ilirejesha imani kwa Ujerumani baada ya vita ingawa amesema imani hiyo inatakiwa kujidhihirisha kila wakati.
Ingawa walitofautiana katika masuala kadhaa lakini waziri mkuu wa Israel Naftali Bennet amemsifu kansela Merkel kwa kuimarisha mahusiano baina ya mataifa hayo na kumuelezea kama Dira ya maadili ya Ulaya kutokana na namna anavyoiunga mkono Israel.
