Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), imedaiwa kuwapo kesi ya ugonjwa wa Ebola Mashariki mwa nchi hiyo.
Kulingana na ripoti kutoka maabara ya taifa ya matibabu ya nchi hiyo ugonjwa huo umezuka ikiwa ni miezi mitano baada ya kumalizika mlipuko mwingine wa hivi karibuni.
Waziri wa Afya wa Congo amekataa kuthibitisha habari hiyo, lakini akasema taarifa itachapishwa hivi karibuni.
Haikujulikana mara moja ikiwa kesi hiyo inahusiana na mlipuko wa 2018 hadi 2020 ambao uliwaua zaidi ya watu 2,200 eneo hilo na wengine sita mwaka huu.
Ripoti kutoka maabara ya biomedical, INRB, ilisema matokeo ya ugonjwa huo yalitoka kwa mtoto wa miaka miwili katika kitongoji chenye watu wengi katika jiji la Beni, moja ya kitovu cha mlipuko wa mwaka 2018 hadi 2020, ambayo ilikuwa ya pili kwa kuua kwenye rekodi.
Watoto watatu majirani wa mtoto huyo walionesha dalili zinazoendana na Ebola mwezi uliopita na kisha kufariki dunia, ripoti hiyo ilisema, lakini hakuna aliyepimwa virusi hivyo.
