Banana flower isolated on white background

Kinamama wanaosumbuka kwa tatizo la kwenda hedhi siku nyingi kinyume cha kawaida wameshauriwa kutumia ua la mgomba kumaliza tatizo.
Mtaalamu wa Virutubisho Tiba, Abdallah Mandai, ameyasema hayo leo Oktoba 11, 2021, jijini Dar es Salaam, wakati akielezea nguvu ya tiba asili katika kupambana na magonjwa mbalimbali.
“Kwa kawaida kipindi cha hedhi ya mwanamke ni kati ya siku nne hadi saba. Siku mbili za mwanzo damu hutoka kwa wingi na baadaye huanza kupungua na hatimaye kuacha.
“Iwapo katika siku zote za hedhi, damu ya itatoka kwa wingi na ikaendelea kutoka hata zaidi ya siku hizo bila kuonesha hali ya kuacha, lazima litakuwa ni tatizo linalohitaji kupatiwa ufumbuzi.
“Pika kichana cha ua la mgomba kula pamoja na glasi moja ya maziwa mtindi. Tumia matibabu hayo asubuhi na jioni kila siku hadi damu zitakapoacha kutoka. Endelea na tiba hii siku mbili baada ya damu kuacha,” ametanabahisha Mtaalam huyo.
Hata hivyo, Mtaalam Mandai amesema ni vema mgonjwa kabla hajatumia tiba hii afike katika kituo chake cha kutolea huduma za afya Ukonga Mongo la Ndege, Dar es Salaam ambapo atapata maelezo ya kina ya namna bora zaidi ya kutumia.

