UHAMIAJI YAELEZA KUZUIWA KWA GODBLESS JONATHAN LEMA MPAKANI
Idara ya Uhamiaji imetoa taarifa kwa umma ikieleza kuwa leo tarehe 6 Juni, 2025, katika Kituo cha Uhamiaji cha mpaka wa Namanga, Arusha, Godbless Jonathan Lema alizuiwa kutoka nchini na pasipoti yake ikashikiliwa.
Taarifa hiyo, iliyosainiwa na S/SI. Paul J. Mselle, Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, imeeleza kuwa Lema anatakiwa kuripoti katika ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Idara imefafanua kuwa utaratibu uliotumika kumzuia Lema kutoka nchini ni wa kawaida na unatumika kwa raia yeyote pale ambapo Idara imepata taarifa zinazohitaji mhusika kuhojiwa.
Aidha, Idara ya Uhamiaji imetoa wito kwa wananchi kupuuza taarifa za uongo zilizochapishwa na Ndugu Lema kupitia mitandao ya kijamii, zikidai kuwa zuio hilo linalenga viongozi wote wa CHADEMA.

Like
Comment
