Rais Samia Suluhu Hassan amewatakia Waislamu na Watanzania wote kheri ya Sikukuu ya Eid al-Adha, akisisitiza mafundisho ya sikukuu hiyo yanayohimiza utii kwa Mola wetu, ukweli, na kumtegemea Mwenyezi Mungu. Rais Samia ameongeza kuwa Sikukuu hii inatufundisha kujali wenye uhitaji na wale wote ambao Mola amewaweka katika njia ya kuhudumiwa.
Aidha, Rais Samia ameiomba Sikukuu hii iendelee kuwa chanzo cha kudumisha amani, upendo, na umoja katika Taifa letu. Amewaombea Watanzania dua njema, akimuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu aendelee kuzikubali na kuzipokea dua zao kwa ajili ya mema ya nchi yetu.
