
Mtaalam wa virutubisho tiba, Abdallah Mandai, amesema ugonjwa wa matubwitubwi ambao mara nyingi huwakumba watoto unatibiwa kwa tangawizi.
“Changanya na maji kidogo unga wa tangawizi kavu kijiko kimoja ili kupata ujiuji mzito, paka uji huo sehemu zote za uso zilizovimba, acha hadi ukauke, osha uso baada ya saa moja na nusu.
“Fanya hivyo asubuhi, mchana na jioni muda wa siku tatu hadi tano, mgonjwa atakuwa amepona tatizo lake,” amesema Mtaalam Mandai, leo Jumanne, Agosti 16, 2022 jijini Dar es Salaam.
Ameongeza kuwa ugonjwa huo unaosababishwa na virusi hushambulia vijifuko vya kutengeneza mate na mara chache unaweza kujitokeza sehemu nyingine za mwili.
Mgonjwa anaposhambuliwa na virusi hao, huvimba sehemu ya chini ya mashavu na wakati mwingine mashavu yenyewe. Uvimbe huo huambatana na maumivu yasiyo makali.
Amesema matubwitubwi ni ugonjwa wa kuambukiza ambao huwapata zaidi watoto wenye umri wa kati ya miaka mitano hadi 15. Si rahisi mgonjwa kuugua tena ugonjwa huo akishaugua mara moja.
