V
Klabu ya Simba, @ahmedally_ amekiri mara baada ya mchezo wa leo kwamba mpinzani wao, Gaborone United, alikuwa na kiwango bora zaidi. Hata hivyo, aliwahakikishia mashabiki kuwa hawana haja ya wasiwasi na kuwa waangalifu, akiwashauri kuwa watulivu katika kipindi hiki cha changamoto.
@ahmedally_ pia amesisitiza kuwa Simba ni klabu kubwa yenye historia na uwezo mkubwa, hivyo katika mashindano haya watatumia ukubwa na umahiri wao kuhakikisha wanashiriki kikamilifu na kufikia malengo ya klabu.
