
Nchi 27 duniani ambazo hazikuwahi kuwa na ugonjwa ndui ya nyani unaofahamika kwa lugha ya kigeni kama MonkeyPox, zimeambukizwa ugonjwa.
Shirika la Afya Duniani (WHO), limethibitisha watu780 kuambukizwa ugonjwa huo usio wa kawaida katika mataifa hayo.
Takwimu za hivi punde hazijumuishi maambukizi katika nchi za Kiafrika ambazo kwa kawaida hukumbwa na maradhi hayo.
Katika taarifa yake shirika la WHO limesema kwa sasa, hatari ya afya ya umma katika ngazi ya kimataifa inatathminiwa kuwa ya wastani ukizingatia hii ni mara ya kwanza kuripotiwa kwa virusi hivyo.
Hakuna aliyefariki kati ya watu hao 780 walioambukizwa. Hadi sasa watu 66 wamefariki dunia katika nchi tano za Afrika kutokana na ugonjwa huo.
