Rais wa Senegal Macky Sall ametoa mwito wa kuondolewa vikwazo dhidi ya Zimbabwe katika hotuba yake kwenye Mkutano Mkuu wa 77 wa Umoja wa Mataifa mjini New York.
Kiongozi huyo wa Senegal, na mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika, amesema hatua kali dhidi ya Zimbabwe zinazidisha mateso kwa watu.
Sall alikuwa kiongozi wa kwanza wa Afrika kuhutubia Baraza Kuu. Alilitaka Baraza la Usalama kushughulikia mizozo barani Afrika kwa njia sawa na kushughulikia mizozo mingine.
Pia ametoa mwito wa mageuzi katika baraza hilo ambayo yatalifanya kuwashirikisha zaidi na pengine kuipa Afrika kiti cha kudumu.
Rais huyo alitoa mwito kwa Afrika kupewa kiti katika kundi la G20, linalojumuisha viongozi wa mataifa 20 makubwa kiuchumi duniani.
Viongozi zaidi wa Afrika wanatarajiwa kuhutubia mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa leo Jumatano katika siku ya pili ya mjadala huo wa ngazi ya juu.
ametoa mwito wa kuondolewa vikwazo dhidi ya Zimbabwe katika hotuba yake kwenye Mkutano Mkuu wa 77 wa Umoja wa Mataifa mjini New York.