
Mtaalam wa tiba asili na virutubisho tiba, Abdalla Mandai amesema juisi ya majani ya ngano ni tiba kwa wenye mwosho wa ngozi.
“Kunywa juisi inayotokana na majani ya ngano asubuhi kabla hujala chakula cha aina yoyote. Baada ya kunywa juisi hii, paka pia majani ya ngano yaliyopondwa kwenye sehemu yenye mwasho,” amesema mtaalam Mandai leo Jumanne, Septemba 2022, jijini Dar es Salaam.
Aidha, Mtaalam huyo amesema kuwashwaa sehemu yoyote ya mwili kunaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali kama minyoo au mzio.
“Kimsingi kuwashwa kunaweza kuwa ni dalili ya ugonjwa unaohitaji uchunguzi na kisha kupatiwa tiba yenye uhakika badala ya kutibu dalili za ugonjwa pekee.
“Hivyo, ni vema ukafanya uchunguzi ili kubaini tatizo kisha uanze tiba. Pia unaweza kutumia majani ya ngano kama nilivyoelekeza kwa kuwa ni msaada mkubwa hususan unapotumia katika hatua za awali za tatizo,” amesema.

Mtaalam Mandai amesema ni vema kila mmoja anapotumia kinywaji cha aina yoyote ili kumwondolea tatizo furani mwilini, azingatie maelekezo ya namna ya kutumia anayopewa na mtaalamu badala ya kuongeza au kupunguza.
“Juisi ya majani ya ngano ni miongoni mwa vinywaji muhimu kwa mwenye tatizo la kuwashwa mwili. Ukinywa juisi hii inasaidia kutengeneza mazingira ya mwili kutohamasishi ukuaji wa bakteria wanaosababisha mwasho wa ngozi ya mwili wa binadamu,” amesema.
