Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 41 wamelazwa hospitalini baada ya kula chakula kinachodaiwa kuwa na sumu katika sherehe iliyofanyika Kijiji cha Kijiji na Kata ya Unyambwa, Wilaya ya Manyoni, mkoani Singida.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, tukio hilo lilitokea Oktoba 17, 2026, majira ya saa 8:00 mchana. Baada ya kula chakula hicho, watu 41 walipata madhara na kukimbizwa katika Hospitali ya Manyoni kwa matibabu.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa hadi Oktoba 18, majira ya saa 05:00 asubuhi, watu 41 walikuwa wamelazwa hospitalini, huku mtu mmoja akiwa amefariki dunia. Kati ya wagonjwa hao, watu 40 walikuwa wamelazwa katika Hospitali ya Manyoni, huku mmoja akihamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida kwa matibabu zaidi.2m