Mpinzani Kabera wa Rwanda mwenye umri wa miaka 50 na mkosoaji mashuhuri wa Rais Paul Kagame wa Rwanda, alikutwa amefariki dunia mjini Kampala mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa hana kichwa. Jeshi la . Polisi liliripoti Jumapili kuwa kichwa chake bado hakijapatikana, jambo lililozua hofu ya mauaji hayo ya kisiasa na ya kikatili sana.
Tukio hili linafuatia mfululizo wa vifo vya kutatanisha na kutoweka kwa wapinzani wa Rwanda wanaoishi nje ya nchi, hasa Afrika Mashariki. Wakosoaji mara nyingi huishutumu serikali ya Rwanda kwa kuwalenga wapinzani wake nje ya mipaka yake.
Mauaji haya yanazua wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wa wakimbizi wa kisiasa nchini Uganda na ukanda mpana wa Afrika Mashariki. Inaweza kuzidi kuzorotesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Uganda na Rwanda, na kuathiri utulivu wa kikanda. Serikali ya Rwanda mpaka tunakwenda mitamboni ilikuwa haijasema chochote kuhusu mauaji hayo ya kutisha.
