Rais Samia Suluhu Hassan hii leo Novemba 17, 2025 ametangaza Baraza la Mawaziri huku akiwaweka kando baadhi ya mawaziri vigogo waliokuwemo kwenye baraza lililopita.
Walioachwa kwenye baraza hilo jipya na wizara zao walizoziongoza kwenye baraza lililopita ni aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt Doto Biteko, Hussein Bashe (Kilimo), Innocent Bashungwa (Mambo ya Ndani) na Jenista Mhagama (Afya).
Wengine ni Dkt Seleman Jafo (Viwanda na Biashara), Dkt Pindi Chana (Maliasili na Utalii) na Dk Damas Ndumbaro wa Katiba na Sheria.
Baada ya kuachwa kwenye uwaziri ni Dhahiri kwamba hawa wote sasa wanabaki na nafasi zao za ubunge na watakuwa wanakaa viti vya nyumba bungeni (back benchers).44s