Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu Ado, amethibitisha kuunga mkono uteuzi wa Mheshimiwa Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema hayo leo Bungeni wakati wa Hoja ya Azimio la Bunge kuthibitisha uteuzi huo, akibainisha sifa ya msingi iliyomsukuma Rais kuchagua Mwigulu.
“Ninasimama kuunga mkono hoja ya pendekezo la uteuzi wa Mheshimiwa Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu. Sifa ambayo nina uhakika nayo ni kwamba Mwigulu Nchemba ni mtu mchapakazi, Kwahiyo, kwetu sisi tulio wachache, tunakuunga mkono kama ishara ya kukukopesha imani tukiwa na uhakika kwamba utachapa kazi.
Tunaamini kwamba utasimamia serikali vizuri katika usimamizi wa rasilimali za taifa na kuwaletea wananchi maendeleo.” amesema Ado.
