Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitisha Dkt. Mwigulu Nchemba, kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwigulu amethibitishwa kwa kura za Ndio 369 kati ya kura 371 zilizopigwa huku za Hapana zikiwa 0, zilizoharibika zikiwa 2.
Uthibitisho huo unafuatia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kumteua Waziri huyo wa zamani wa Fedha na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mkoani Singida kwenye nafasi hiyo.
