
Maziko ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa na Meneja wa kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Chalinze, Stivin Kazidi yanafanyika leo, Januari 3, 2022.
Mzee Kazidi maarufu kama Biko, alifariki dunia usiku wa kuamkia jana Januari 2, 2022 katika Hospitali ya Mloganzila alikokuwa akipatiwa matibabu.
Mazishi ya ya Biko yanatarajiwa kufanyika leo Januari 3, 2022 saa 7 mchana baada ya swala ya adhuhuri, kwenye makaburi ya familia yao yaliko Vigwaza.
Msiba wa Mzee Biko upo nyumbani kwake Vigwaza Kambini, mkoani Pwani.
