MANCHESTER, ENGLAND - AUGUST 30: Bryan Mbeumo of Manchester United celebrates scoring his team's second goal during the Premier League match between Manchester United and Burnley at Old Trafford on August 30, 2025 in Manchester, England. (Photo by Matt McNulty/Getty Images)
Manchester United inasikitisha kwani imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Leeds United katika mchezo wa Ligi Kuu England, licha ya kuonyesha juhudi zaidi kwa kutumia mfumo mpya wa uchezaji, huku presha dhidi ya kocha Michael Carrick ikiendelea kuongezeka.
Katika mchezo huo uliopigwa katika Dimba la Elland Road, Manchester United ilionesha ari na kujituma zaidi, lakini ilishindwa kutumia nafasi hiyo kupata ushindi wa pili wa ligi msimu huu.
United, iliyocheza sehemu kubwa ya mchezo bila mshambuliaji wa asili, ilipata bao la kwanza katika kipindi cha kwanza kupitia Bryan Mbeumo, aliyefunga kwa kushirikiana na wachezaji wenzake baada ya timu hiyo kuonyesha mashambulizi yenye ufanisi.
Hata hivyo, kadiri mchezo ulivyoendelea, Manchester United ilipoteza kasi na kushindwa kuhimili presha ya Leeds, ambayo ilisawazisha kupitia Dominic Calvert-Lewin baada ya kutumia vizuri mpira wa kona uliokuwa haujalindwa ipasavyo na safu ya ulinzi ya United.
Matokeo hayo yanaongeza changamoto kwa Carrick, ambaye timu yake imekuwa na mwenendo usioridhisha katika mechi za mwanzo za msimu huu.
Manchester United imeshinda mchezo mmoja pekee kati ya saba ya Ligi Kuu England msimu huu, huku ikipata sare nne na kupoteza miwili. Huo ni mwanzo wake mbaya zaidi kwa idadi ya ushindi katika hatua hiyo ya msimu tangu msimu wa 1986/87.
Ingawa United ilionyesha kiwango bora zaidi ikilinganishwa na sare yake ya wiki iliyopita dhidi ya Tottenham Hotspur, matokeo hayo bado hayatoshi kupunguza maswali kuhusu uwezo wa Carrick kuiongoza timu hiyo.
Presha kwa kocha huyo inaendelea kuongezeka huku mashabiki wakisubiri kuona mabadiliko ya matokeo na kiwango cha Manchester United katika michezo ijayo.
